Tuesday, June 25, 2013
Sunday, June 23, 2013
KATIKA KISA NA MKASA TAZAMA HAPA CHATU ALIVYOMMEZA MAMA HUYU
chatu ambae alimmeza linda akijihami baada ya wasamalia wema na askari kuwasili eneo la tukio |
Mwanamke mmoja amepoteza maisha mara baada ya nyoka aina ya chatu kuingia nyumbani kwake na kumjeruhi kisha kummeza kabisa wakati waokoaji wanafika katika nyumba ya mama huyo ambaye alijulikana kwa jina la linda laina nyatoro Huko nchini afrika kusini
mwalimu mbaroni kwa kumbaka mwanafunzi wa miaka 10
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea juzi hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
***
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya
linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi
wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
lilitokea Hivi karibunikatika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa
Mbeya.
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa
ni Ipyana Gidion(30),kyusa,mkulima mwalimu wa masomo ya ziada (tuition)
katika kituo cha Itunge Moravian mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10, kyusa,mwanafunzi darasa la nne katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Kamanda Diwani alisema mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
Aliongeza kuwa mtuhumiwa aliwahi
kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka
kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo
taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.(Joseph mwaisango wa Mbeya yetu)
Saturday, June 22, 2013
SHOO YA KILI MUSIC TOUR 2013 NI FUNIKA BOVU DOM .... JIONEE MAMBO YANAVYOENDELEA UKUMBINI, NI HATARIIIII
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linex, akishambulia jukwaa wakati wa
Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour, 'Kwetu ni Kwetu',
lililomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Kwa
habari kamili na mapicha kibao ya shoo hii utapata kupitia ukurasa wa
mtandao huu baadaye. 'Stay Tune'.
Ommy Dimpoz, akishambulia jukwaa...
Msanii wa Hip Hop, Kala Jeremier, akiwarusha mashabiki wake kwa mistari....
Msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki, akiwarusha mashabiki wake kwa mistari....
Shabiki
mwanadada aliyepagawa na miondoko ya Bongo Flava, akiwa na Bukta baada
ya kuvua suruali yake na viatu (kushoto kwake chini) huku akisebeneka na
miondoko iliyokuwa ikirindima jukwaani.
Subscribe to:
Posts (Atom)