Saturday, July 13, 2013

je tutafika kwa hali hiii ni ndani ya mtaaa

ujasiliamali ni hali ya kawaida tujifunze kujituma

791414

Nyama choma kwenye kitanda cha Enzi zileeee


HUYU HAPA NDIE BABU ANAEDAI AONYESHWE NJIA YA KWENDA BUTIAMA AKAMFUFUE MWALIMU NYERERE chukua muda wako kupita hapa na kusoma zaidi.



Mzee (pichani) aliyeibuka hivi karibuni akidai kuwa ana uwezo wa kumfufua Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere amezua gumzo.

 Babu huyo aliibuka katika studio za Kyera FM huko mkoani Mbeya akihitaji msaada wa kumfikisha Butihama alipozikwa Mwalimu Nyerere mwaka 1999 ili amfufue. 


Mzee huyo alikuwa na ufunguo mkononi ambao anadai ndiyo utakaotumika kumfufua Nyerere. Anaeleza kuwa akishamfufua Mwalimu Nyerere ndiye atakayesimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Sunday, June 23, 2013

KATIKA KISA NA MKASA TAZAMA HAPA CHATU ALIVYOMMEZA MAMA HUYU

 

chatu ambae alimmeza linda akijihami baada ya wasamalia wema na askari kuwasili eneo la tukio
 
Mwanamke mmoja amepoteza maisha mara baada ya nyoka aina ya chatu kuingia nyumbani kwake na kumjeruhi  kisha kummeza kabisa wakati waokoaji wanafika katika nyumba ya mama huyo ambaye alijulikana kwa jina la linda laina nyatoro Huko nchini afrika kusini 


Yupo ndani ya mtaa anatafuta mchumba na anaomba ushauri wenu?


mwalimu mbaroni kwa kumbaka mwanafunzi wa miaka 10

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea juzi hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.

***

JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea Hivi karibunikatika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
 
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ipyana Gidion(30),kyusa,mkulima mwalimu wa masomo ya ziada (tuition) katika kituo cha Itunge Moravian   mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
 
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa  miaka 10, kyusa,mwanafunzi  darasa  la  nne  katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
 
Kamanda Diwani alisema  mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha  kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
 

Aliongeza kuwa  mtuhumiwa  aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.(Joseph mwaisango wa Mbeya yetu)

Saturday, June 22, 2013

SHOO YA KILI MUSIC TOUR 2013 NI FUNIKA BOVU DOM .... JIONEE MAMBO YANAVYOENDELEA UKUMBINI, NI HATARIIIII

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linex, akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour, 'Kwetu ni Kwetu', lililomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Kwa habari kamili na mapicha kibao ya shoo hii utapata kupitia ukurasa wa mtandao huu baadaye. 'Stay Tune'.
Ommy Dimpoz, akishambulia jukwaa...
Ben Paul, akifunika baada ya kuimba baadhi ya bibao vyake jukwaani.
Msanii wa Hip Hop, Kala Jeremier, akiwarusha mashabiki wake kwa mistari....
Msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki, akiwarusha mashabiki wake kwa mistari....
Shabiki mwanadada aliyepagawa na miondoko ya Bongo Flava, akiwa na Bukta baada ya kuvua suruali yake na viatu (kushoto kwake chini) huku akisebeneka na miondoko iliyokuwa ikirindima jukwaani.